JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 18
14

MOROGORO: Mwalimu wa Shule ya Msingi Dutumi, Rahaleo Salehe Kazimbaya ajinyonga mara baada ya kumuua Mkewe, Sikilinda Magumba kwa kumchoma na Kisu - Sababu za Mwalimu huyo kuumua Mkewe kisha kujiua yeye mwenyewe bado haijafahamika

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 18
264

KIFO CHA MWANAFUNZI: Serikali imesema imepata pigo na itahakikisha waliohusika wanachukuliwa hatua. - Aidha, imeahidi kugharamia shughuli zote za mazishi ya marehemu hadi atakapopumzishwa katika makao yake ya milele. - Akiongea na Wanahabari, Waziri wa Elimu amewasihi Watanzania kujiepusha na maandamano na vitendo vyote ambavyo vinaweza kusababisha uvujifu wa amani - Na kwa upande wake Naibu Wazi

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 18
17

IRAN: Watu 66 wamefariki baada ya Ndege ya abiria kuanguka kusini mwa nchi hiyo - Hii inakuwa ni ndege ya pili kuanguka katika nchi hiyo katika kipindi cha siku siku 10 - Ndege nyingi za abiria nchini humo zimechakaa kutokana na nchi hiyo kuwekewa vikwazo kwa takribani muongo mmoja sasa

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 18
328

IKULU, DAR: Rais Magufuli amesikitishwa na kifo cha Mwanafunzi wa NIT, Aqulina Akwilini aliyepigwa risasi ktk Maandamano ya CHADEMA - Rais kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter ameviagiza Vyombo vya Dola kuchunguza tukio hilo na kuwachukulia hatua waliohusika kusababisha kifo hicho - Rais pia ametoa pole kwa Familia, Ndugu, Wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT) na wote walioguswa na ms

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 18
50

ZIMBABWE: Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Zimbabwe, Levi Nyagura amekamatwa kwa tuhuma za kumtunuku Shahada za Uzamivu(PhD) Mke wa aliyekuwa Rais wa Nchi hiyo Robert Mugabe - Bi Grace Mugabe alitunukiwa Shahada hiyo baada ya kusoma kwa miezi michache kinyume cha utaratibu huku kukiwa na harufu ya rushwa - Wakufunzi kutoka Idara ya Sosholojia chuoni hapo wamesema kuwa hawajaona nyaraka zozote za kuth

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 18
208

CHADEMA yatangaza kutoyatambua matokeo ya Uchaguzi Mdogo katika Majimbo ya Siha(Kilimanjaro) na Kinondoni(Dar es Salaam) - Kupitia taarufa rasmi ya chama hicho imewaagiza Mawakala wake kutofika vituo vya vikuu ya majumuisho ya kura katika majimbo hayo. - CHADEMA wamedai kuwa Tume ya Uchaguzi katika Jimbo la Kinondoni imefanya urasimu na makosa ya makusudi ili kuhakikisha chama hicho kinakosa Mawak

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 18
105

DAR: Tume ya Uchaguzi(NEC) imemtangaza Maulid Mtulia wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) kuwa mshindi wa Uchaguzi Mdogo wa Ubunge, Jimbo la Kinondoni - Maulid Mtulia amepata kura 30,313 akifuatiwa na mpinzani wake wa karibu, Salum Mwalim(CHADEMA) aliyepata kura 12,353 na Rajab Salum wa CUF aliyepata kura 1,943. - Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, Mkuu wa Mkoa Paul Makond

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 18
68

ILIANDIKWA MIAKA 7 ILIYOPITA; #Repost @macdemelo ・・・ Taratibu Tanzania inabadilika na kuwa “Dola katili ya Kipolisi” mbele za macho yetu na hakuna lolote tunalofanya. Ukatili huu wa Polisi umefikia viwango visivyovumilika nasi tukiwa mashahidi kila siku lakini bado tuko kimya kuhusu hilo. .... Uthubutu wa Polisi wa kupiga na hata kuua raia, wakiwemo wanafunzi, wenye lengo la kujenga uoga na unyam

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 17
184

SIHA, KILIMANJARO: Tume ya Uchaguzi(NEC), yamtangaza Dk Godwin Mollel wa Chama cha Mapinduzi(CCM) kuwa mshindi wa Uchaguzi Mdogo wa Ubunge, Jimbo hilo - Dkt. Mollel amepata kura 25,611 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Elvis Mosi wa CHADEMA aliyepata kura 5,905 #JFLeo #UchaguziMdogo

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 17
419

KINONDONI, DAR: Katika matokeo yanayoendela kutoka mpaka sasa Jimboni hapo Mgombea wa CCM, Said Mtulia anaongoza akifuatiwa na Mgombea wa CHADEMA, Salim Mwalim - Matokeo hayo ya awali ni kama ifuatavyo; Katika vituo 22 ambavyo kura zimehesabiwa, CCM anaongoza katika vituo 21 huku Mwalim akiongoza katika kituo kimoja - SIHA, KILIMANJARO: Katika matokeo yanayoendela kutoka mpaka sasa Jimboni hapo Mg

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 17
52

Serikali kupitia kwa Waziri wa Mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba, imeliagiza Shirika la Wakimbizi(UNHCR) kuongeza kasi ya kuwarudisha kwao raia wa Burundi zaidi ya 34,000 walioko katika kambi za wakimbizi mkoani Kigoma - Wakimbizi hao wapo katika kambi za Nduta, Nyarugusu na Mtendeli, na waliomba kwa hiari yao kurudishwa kwao

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 17
268

NKASI, RUKWA: Mwalimu Mkuu wa shule sekondari Kabwe, Jackson Mussa amemkaba koo na kumpiga makofi Mwalimu wa Jiografia, Emmanuel Mbemba mbele ya Wanafunzi - Mwalimu Mbemba alikwenda ofisini kwa Mkuu wa shule kuomba ruhusu ili awapeleke Wanafunzi kwenye ziara ya mafunzo kwa kutembelea fukwe za Ziwa Tanganyika - Mkuu huyo wa shule alimtaka mwalimu huyo aandike barua ya kiofisi na alifanya hivyo. Ali

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 17
47

Kituo hicho cha Idrisa Kata ya Magomeni ndipo inapodaiwa kuwa sanduku la kupigia kura liliibiwa na lilirejeshwa na Polisi wakiwa na mtu aliyeiba - Tukio hili lilikanushwa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Kituo hicho, Zuhura Mohamed #UchaguziMdogo

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 17
214

Mgombea ubunge Kinondoni (CHADEMA), Salum Mwalim amekamatwa na Polisi katika kituo cha kupigia kura cha Idrisa kata ya Magomeni - Salum Mwalim alidai katika kituo hicho kuna boksi la kura liliibiwa na kurudi tupu, hivyo alitaka uchaguzi usitishwe kituoni hapo - Inasemekama sababu ya Kukamatwa kwake ni kufika kituoni hapo na kundi kubwa la Watu - UPDATE: Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni, Salum

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 17
892

DAR: Kamanda Lazaro Mambosasa amekiri mtu mmoja kupigwa risasi na Polisi wakati wakiwatawanya wafuasi wa CHADEMA walioandama jana Februari 16, 2018 - Wafuasi wa Chadema wakiongozwa na Freeman Mbowe waliandamana kuelekea ofisi ya msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Kinondoni, Aron Kagurumjuli kudai viapo vya mawakala wa chama chao - Maandamano hayo yalianzia viwanja vya Buibui Mwananyamala ulikokuwa uki

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 17
182

SIHA, KILIMANJARO: Mawakala 67 kati ya 70 wa Usimamizi wa Uchaguzi mdogo wa Chama cha Wananchi(CUF ), watolewa vituoni kwa madai kuwa barua zao za kiapo zimesainiwa na Msimamizi Uchaguzi wa jimbo hilo badala ya Hakimu - KINONDONI, DAR: Mawakala katika vituo mbalimbali vya kupigia kura wametolewa nje kwa sababu tofauti. Huku zoezi la upigaji kura likiendelea #JFLeo #UchaguziMdogo

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 17
213

ARUSHA: Madiwani watatu katika Wilaya Ngorongoro wamejiengua CHADEMA na kuhamia CCM kwa ridhaa yao - Madiwani hao ni Diwani Daniel Orkeriy(Ngorongoro), Mwenyekiti wa Vijana wa CHADEMA wa Wilaya na pia Diwani wa Kata ya Ngoile, Lazaro Saitoti na Diwani Sokoine Moiv(Loitole) - Viongozi hao walisema kujiengua kwao kumetokana na kukengeuka na kujikuta wakiwa CHADEMA bila kutafakari na uamuzi huo umewa

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 17
14

Leo Februari 17 ni siku ya kupiga kura katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika majimbo mawili ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na Siha mkoani Kilimanjaro - Pia unafanyika Uchaguzi mdogo wa Madiwani katika Kata 8 za Tanzania Bara - Uchaguzi huu utahusisha jumla ya wapiga kura 355,131 walioandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura na kutakuwa na vituo vya kupigia kura 867

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 16
42

Serikali ya Ethiopia imetangaza hali ya hatari(State of Emergency) nchini humo ikiwa ni siku 1 toka ajiuzulu Waziri Mkuu wake, Hailemariam Desalegn - Vyombo vya habari vya ndani ya nchi hiyo vinasema haijawekwa wazi ni kwa muda gani hali hiyo itachukua kuisha - Inadaiwa Baraza la Mawaziri lilikuwa linabishana sana kuamua kama hali hiyo ichukue muda wa miezi mitatu au sita - Mwaka 2015, Ethiopia il

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 16
20

Mjadala kutoka JamiiForums: Ipo dhana kuwa mume na mke wote wakiwa na kipato, basi kipato cha mume ndio kitatumika kugharamikia matumizi ya familia kama chakula, kodi, kusomesha watoto na mengineyo. Huku kipato cha mke kutoguswa kabisa. - Una maoni gani juu ya Dhana hii?

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 16
81

Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) wamekubaliana kugoma Aprili 1, 2018 ikiwa hawatalipwa madai yao zaidi ya billion 2 - Majina ya Wanataaluma 140 ndio yametoka katika orodha ya wanaostahili kulipwa, japo zaidi ya Wanataaluma 500 wanadai - Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Shukuru Mlwafu, amewalaumu baadhi ya watendaji wa serikali, hasa wanaomsaidia Rais Magufuli kwa karibu kuwa wanamp

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 16
43

Serikali kupitia Waziri Dkt. Mwigulu yamuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi, kufanya uchunguzi wa mauaji ya Katibu Kata wa Hananasif - Kinondoni, Dar - Waziri Nchemba amesema kuwa maswala ya Demokrasia huamuliwa kwa peni na karatasi na si kwa Panga, Rungu wala Mkuki - Waziri Dtk. Mwigulu Nchemba ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani amelitaka Jeshi la Polisi kuchunguza kwa kina tukio hilo na kujua undani

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 16
20

Serikali ya Tanzania imezuia usafirishaji wa Makontena kwenda Zanzibar kupitia Bandari ya Mombasa Kenya - Inaelezwa kuwa TRA imeiandikia Serikali ya Kenya na kuiambia katika uongezekaji wa kuingizwa kwa bidhaa kimagendo Tanzania, chanzo chake kimeonekana ni Makontena yanayoingia kupitia bandari ya Mombasa - Makontena 264 ambayo yalikuwa yaende Zanzibar yamezuiwa nchini Kenya katika bandari hiyo y

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 16
54

Kampuni itoayo huduma katika mradi wa mabasi ya mwendokasi (UDART) imeongeza mabasi 70 kutoka China - Mkurugenzi Mtendaji wa UDART, Charles Newe amesema mabasi hayo yatakuwa na uwezo wa kubeba abiria 150 hadi 160. Ujio wa mabasi hayo kunafanya idadi yake kufikia 210 - Aidha, amesema ujio wa mabasi haya utawafanya watu wayaache nyumbani magari yao na kupunguza gharama kutoka Sh 8,000 hadi Sh 2,000

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 16
34

KILOLO, IRINGA: Mahakama yamhukumu kifungo cha maisha jela, Frank Mlyuka kwa hatia ya kubaka na kulawiti Mtoto wa Kike wa miaka 3 - Kijana huyo mwenye umri wa miaka 24 ametakiwa kulipa Tsh. Milioni 5 kama fidia kwa Wazazi wa Mtoto huyo - Mwendesha mashtaka wa Serikali, amesema kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo mnamo Februari 9, 2018 katika Kijiji cha Kihesa Mgagao. Ambapo Kijana huyo alimmwingiz

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 16
113

MOSHI: Mahakama Kuu imemhukumu kifungo cha maisha jela raia wa Lithuania, baada ya kumpata na hatia ya kusafirisha #DawaZaKulevya - Christina Biskasevskaja(26) alikamatwa na #DawaZaKulevya aina ya Heroin na Hydrochloride zenye uzito wa Gramu 3775.26 na thamani ya Tsh Mil 169,886,700 - Binti huyo ambaye pia ni Mwanamuziki alikamatwa Agosti, 28 mwaka 2012 katika Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA)

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 16
291

INDIA: Mtanzania Brayton Lyimo amekamatwa Uwanja wa Ndege wa Indira Gandhi(IGI) akisafirisha Dawa za Kulevya zenye thamani ya Shilingi Milioni 351 - Kijana huyo amekamatwa akiwa na Kilogramu 4.8 za #DawaZaKulevya aina ya Heroine - Je, nini kifanyike ili vijana wa Kitanzania waachane na biashara hii inayochafua taswira ya Tanzania kimataifa?

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 16
195

Mtoto wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 2 na miezi 9 amerudishwa nchini baada ya Wazazi wake kuhukumiwa kifo nchini China baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha #DawaZaKulevya. - Baraka Malali ambaye ni Baba wa Mtoto huyo alitoa kwa njia ya haja kubwa pipi 47 na Ashura Musa ambaye ni Mama yake alitoa pipi 82 za dawa hizo haramu - Watanzania hao walikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Baiyun uliop

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 16
12

IKULU, DAR: Rais Magufuli anatarajiwa kuwaapisha Mabalozi 2 aliowateua. Dkt. Slaa Balozi nchini Sweden na Muhidini Mboweto Balozi nchini Nigeria - Uteuzi Wa Mabalozi hao kuiwakilisha Tanzania katika nchi hizo(Nigeria & Sweden) umeanza jana 15 Februari

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 16
544

DAR: Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Jumanne Muliro amesema Jeshi hilo limemchukulia hatua za kinidhamu Askari Polisi aliyeonekana katika picha ya video akichukua rushwa #JFLeo #corruption

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 15
51

Mjadala Kutoka JamiiForums: Wakuu wa Mikoa na Wilaya wamekuwa wakiwakamata wanafunzi wanaopata mimba ili kuwashininikiza kuwataja watu waliohusika kuwapa mimba - Wadau mbalimbali wamekosoa hatua hii na kusema sio njia sahihi na inakiuka haki za mwanafunzi - Una maoni gani juu ya swala hili?

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 15
19

SHINYANGA: Mechi kati ya Mwadui FC na Simba SC imemalizika. Matokeo ya mechi hiyo ni kwamba Mwadui FC na Simba SC wametoka suluhu ya goli 2 kwa 2 - Suluhu hii imewafanya Simba wafikishe alama 42 baada ya mechi 18 huku ikiendelea kuongoza ligi kwa tofauti ya alama 5 - Magoli ya Simba SC yamefungwa na John Bocco(9’) na Emmanuel Okwi(71’). Mwadui ambayo ilitoka nyuma mara mbili na kusawazisha, magol

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 15
53

Mwenyekiti CHADEMA Freeman Mbowe na viongozi wengine wa chama wamekwenda ofisi ya NEC kushinikiza wapewe viapo na vitambulisho vya mawakala wao, huku wakidai mawakala wa CCM wameshapewa - Msafara huo wa viongozi ulipofika ofisi hizo kwa lengo la kukutana na Mkurugenzi wa Tume hiyo, Ramadhan Kailima waligonga mwamba baada ya watumishi wa NEC kudai kuwa Mkurugenzi huyo hayupo ofisini - Viongozi hao

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 15
100

Idara ya Serikali ya Marekani imetangaza kuwa Washington watazipa adhabu za kibiashara nchi za Afrika Mashariki ambazo zipo katika mkakati wa kusimamisha uingizwaji wa nguo zilizotumika(mitumba) - Washington wanaona Mkakati huo wa kusimamishwa uingizwaji mitumba ni kama uzuiaji wa biashara huria - Harry Sullivan, kiongozi wa Kitengo cha Uchumi na mambo ya Kikanda katika Idara ya Maswala ya Afrika

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 15
29

AFRIKA KUSINI: Makamu wa Rais, Cyril Ramaphosa amechaguliwa na Bunge kuwa Rais mpya wa nchi hiyo baada ya Jacob Zuma kujiuzulu - Jaji Mkuu wa Nchi hiyo, Mogoeng Mogoeng anatarajiwa kumuapisha kushika wadhifa huo hadi Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwakani(2019) - Aidha, Ramaphosa baada ya kuchaguliwa analihutubia Bunge la Nchi hiyo muda huu

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 15
41

ETHIOPIA: Waziri Mkuu Hailemariam Desalegn atangaza kujiuzulu kutokana na mgogoro wa kisiasa uliosababisha vifo vya mamia ya raia - Katika taarifa yake amesema kuwa kujiuzulu kwake kutasaidia kuleta mabadiliko ya kiutawala na kukuza amani - Ameongeza kuwa atasalia kama kiongozi muangalizi hadi pale chama chake cha EPRDF ambacho ni chama tawala na Bunge la Taifa hilo watakapokubali kujiuzulu kwake

JamiiForums @jamiiforums on Instagram photo February 15
27

NAIROBI, KENYA: Mahakama Kuu imetangaza kuwa ufukuzwaji wa Mwanasheria na Kiongozi wa NRM, Miguna Miguna ni kinyume cha sheria na kuwa Miguna yupo huru kurejea nchini humo - Ikiwa ni siku 9 tangu aondoshwe nchini humo, leo Jaji wa Mahakama Kuu, Justice Luka Kimaru ameiagiza Serikali kupeleka hati ya Kusafiria ya Miguna Mahakamani hapo ndani ya siku 7 - Saa chache baadaye, Serikali imejibu na kusem

Popular Now

منزل شیک من💒💐 @manzele_shike_man on Instagram photo February 18
+ Board

. عکسها رو ورق بزنید . منزل دوست عزیز از تهران . متراژ منزل ۱۰۰ متر _______________ لطفا شما هم عکسهای منزلتون رو به لینک تلگرام بالای صفحه ارسال کنید

Cocoa Swatches @cocoaswatches on Instagram photo February 18
+ Board

Revisiting the bronzer convo and added a few contour powders in the mix. What’s missing from the list? Which is your fave? Mattes (T to B) ⚡️ @bobbibrown bronzer in deep 4 ⚡️ @marenabeaute powder in Ebéne ⚡️ @blackradiancebeauty powder in Ebony (contour) ⚡️ @maccosmetics sculpting powder in Definitive (contour) ⚡️ @makeupforeverus artist face powder in S118 (contour) ⚡️ @makeupgeekcosmetics conto

کیف وکفش لنگه به لنگه(اندیمشک) @kif_kafsh_lenge_be_lenge on Instagram photo February 18
+ Board

. . کیف دستی و پاسپرتی کنفی😍 . . ★★برای اطلاع از قیمت به کانال تلگرام مراجعه فرمایید.لینک تو بیو👆👆 * . . . * ❌توی کامنت قیمت داده نمیشه.لطفأ قیمت نپرسید❌ * * #کفش_زنانه#کیف #کفش_عمده #عمده#کوله #کوله_پشتی #کوله_مدارس#نیمبوت #نیم_بوت #اندیمشک #دزفول #اهواز#andimeshk #andimeshk_city dezful #dez #dezful #لنگه_به_لنگه #lenge_be_lenge

Piatã FM @piatafm on Instagram photo February 18
+ Board

O #EspecialPiatãFM de hoje vai ser com a banda que promete ser umas das melhores do nosso MAIOR FESTIVAL DE SAMBA DO MUNDO 🌎. A banda @imaginasambaoficial vai fazer a sua festa no #EsperandoOSambaPiatã. 🎧🎤🎶ㅤ Então não fique de fora e venha curtir com a gente!🙌🏾ㅤ ㅤ Sintonize 📻 94.3, acesse 💻 www.piatafm.com.br ou 📱 baixe o app grátisㅤ ㅤ #EmpurraPiatã #PiatãFM #RádioDaGente #PrimeiroLugar #ComeçaCom